zaterdag 27 oktober 2012

SHEREHE ZA EID EL HAJJ ZILIVYOFANA NCHINI BELGIUM (PART 1)

Mama Kareem mwenye ushungi mweusi nyuma akiwa na wageni wake waalikwa kwenye sherehe za Eid El Hajj zilizofanyika jana nchini Belgium.

Baadhi ya wageni waalikwa toka nchini Holland waliofika ukumbini wakisikilza mawaidha kwa makini

Kicheko cha furaha kwa wageni wetu toka nchi mbalimbali duniani waliokubali wito wetu na kujumuika pamoja nasi kwenye sherehe za Eid El Hajj hapo jana

Kikosi kazi ambacho kilihakikisha kila jambo linakwenda sawa,Big Up kwa Jembe Ally kushoto,Big Up kwa Dulla,Big Up kwa Jembe langu A.  na Big up kwa baba Talha kulia.

Baba Kareem katikati akiwa na wageni wetu waaalikwa kwenye sherehe za Eid El Hajj hapo jana.

Maganga One Blogger mwenye shati la pupple nikiwa na wageni wetu waalikwa kwenye sherehe zetu za Eid El Hajj hapo jana.
Aunt Josee kulia akipata picha ya kumbukumbu

Dada zangu wakipata picha za kumbukumbu za sikukuu ya Eid el Hajj nchini belgium hapo jana.
Mama Sharon mwenye Pupple akipata picha na wageni wetu waalikwa kwenye sikukuu ya Eid hapo jana.
Wageni wetu wakisikiliza mawaidha ya Eid El Hajj hapo jana,tunawashukuru sana wageni wetu wote waliopokea wito wa sherehe hizi na Allah atawalipa kwa wema wenu insh`Allah.

maandag 27 augustus 2012

SIKUKUU YA EID EL FITR TULIVYOISHEHEREKEA NCHINI BELGIUM

Kina dada watanashati wakisikiliza kwa makini mmoja wao alipokuwa akisoma Quran tukufu siku ya Eid El Fitr.
Bi dada Sharon akisoma Quran tukufu huku mkononi akiwa ameshikilia fedha ambazo alikuwa akitunzwa na walioguswa pale alipokuwa akisoma.
Kushoto ni bidada Cherie akiwa na bidada Moza walipokuwa wakisoma na kutafsiri Quran siku ya Eid
Huyu ni kaka Kareem ambaye hakubaki nyuma katika usomaji wa Quran..
Bidada Cherie
Bidada Moza
Kaka Nabil
Mwalimu wa Madrassa kushoto akiwa na wanafunzi wake wakipata picha pamoja kuweka kumbukumbu.
Keki maalumu ya Eid
Ukiiangalia keki vyema utaiona jinsi ilivyochanganywa kitaalamu zaidi kwa matunda
Wageni mbalimbali walihudhuria sherehe za Eid siku hiyo
Kila mmoja alikuwa bize kupata sadaka ya Eid

Ndugu,jamaa na marafiki walijumuika pamoja katika sadaka ya Eid..
Kwa upande wa kina mama nao hawakubaki nyuma,tunashukuru kwamba walitupa sapoti
Madada nao......
Sherehe yetu ilipendeza mash`Allah